islamkingdomface islamkingdomtwitte islamkingdominstagram islamkingdompinterest islamkingdomtumblr islamkingdomreddit islamkingdomvk


IKHLAS ( KUMTAKASA MWENYEZI MUNGU SUBHANA WA TAALA)


9106
wasifu
muislamu atakikana amali zake zote anazo fanya awe na ikhlas katika amali ile nao nikufanya kwa ajili ya kutaka radhi za mwenyezi mungu peke yake wala sikufanya kwa ajili ya ria na kutaka kusifiwa,na amali yoyote mwanadamu atakae ifanya kwa kutaka kujionyesha ama kutaka kusifiwa basi mja huo hatalipwa siku ya kiyama na matendo yake yatakuwa yameruka patupu.
Khutba ya

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Aliyetujaalia sisi ni katika umma bora, umma wa Mtume Muhammad (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Na hapana apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa yeye peke yake, hana mshirika katika ibada, hakuzaa wala hakuzaliwa. Sala na Salamu zimfikie Mtume wake Aliye tumilizwa kuwa ni rehma na amani kwa viumbe vyote. Sala na Salamu ziwafikie Jamaa zake na Sahaba zake wote.

Kabla ya kuingia katika maudhui, tunataka tueleze Nini Ikhlasi? Ikhlasi ina maana nyingi; Kuna wanao sema: Ikhlasi ni kuwa sawa ndani ya mwanaadamu na nje yake. Wengine wasema: Ikhlasi n ikufanya vitendo bila yakujionesha. Na mtu yoyote anayefanya vitendo vyoyote bila ya kujitakasa, vitendo vyake havikubaliwi. Kwasababu Ikhlasi ni nguzo muhimu ya kukubaliwa vitendo.

Enyi Waja wa Mwenyezi Mungu, hakika Ikhlas ni jambo ambalo havikubaliki vitendo vya mtu inapokosekana. Na kwa sababu ya Ikhlas huzidishiwa daraja mtu.

Enyi waja wa Mwenyezi Mungu Ikhlas ni jambo kubwa, nayo ni katika nguzo za kukubaliwa vitendo. Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) hakubali vitendo ila viwe ni vyema vimefanywa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Mwenye kufanya vitendo na akamshirikisha Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) kwa kumkusudia mtu mwengine asiyekuwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala), Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) hakubali amali yake, hata amali hiyo iwe nyingi kiasi gani. Dalili katika hayo ni maneno yake Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Aliposema:

قال تعالى : (إِنَّا أَنْزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ فَاعْبُدِ اللَّهَ مُخْلِصًا لَهُ الدِّينَ أَلَا لِلَّهِ الدِّينُ الْخَالِصُ)[الزمر: 2] {{Hakika sisi tumekuteremshia Kitabu hiki kwa haki, basi muabudu Mwenyezi Mungu, kwa kumfanya Mola yeye tu Wakuitakidiwa Mola ni Mwenyezi Mungu pekeyake}} [ Az-zumar 2-3].

Enyi Waislamu jueni ya kuwa vitendo vyote lazima viwe na (Ikhlas) kujitakasa. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

وقال) : قُلْ أَمَرَ رَبِّي بِالْقِسْطِ وَأَقِيمُوا وُجُوهَكُمْ عِنْدَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَادْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ كَمَا بَدَأَكُمْ تَعُودُونَ) [الأعراف: 29]

{{Sema: Mola wangu ameniamrisha uadilifu, na elekezeni nyuso zenu kwake wakati wa kila sala na muabuduni yeye tu kwa utii khalisi kama alivyo kuumbeni kwanza}} [A- Araf : 29].

Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

وقال) : وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ وَذَلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ ) [البينة: 5]

{{Na wala hawakuamrishwa ila kumuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia dini, waache dini za upotofu}} [.Bayyina: 5].

Sifa na vitendo vyote vilivyo mbali na ikhlasi havikubaliwi na Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Ewe mja wa Mwenyezi Mungu ni kukusudia vitendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu peke yake wala usimshirikishe na chochote ndio utapata malipo kutoka kwa Allah.

Zingatia Ewe Muislamu ni vipi Qur’an ina muombea mwenye kuisoma, pamoja na kuwa Qura’n ni maombezi siku ya kiyama lakini hapa haikumuombea kwa sababu ya kukosa ikhlas. Ni hivyo hivyo mali hayamuombei mwenye mali kwa kufanyia watu wema kuunga kizazi kwa sababu ya kukosa ikhlas. Na vile vile aliyepigana vita lakini kupigana kwake hakukumsaidia Allah. Kwa sababu alikuwa mbali na ikhlas. Je mimi na wewe tuko wapi? Ole wetu tukihalifu ikhlas ambayo ni nguzo kubwa ya kukubaliwa vitendo.

Mambo yanayo haribu Ikhlas:

a. Kumshirikisha Mwenyezi Mungu sawa kwa shiriki ndogo au kubwa. (1) Shirki kubwa : Ni kuthibitisha mshirika wa Mwenyezi Mungu kwa kukusudiwa mwingine. Na Shirki hii inamtoa mtu kwenye dini, na kwasababu ya shirki ataingia motoni na atabaki humo milele na shirki kubwa hubatilisha na kuharibu vitendo yote. (2) Shirki ndogo: nayo ni kila neno au kitendo kilicho kusudiwa kuonyesha watu. Shirki haimtoi mtu katika dini kama kujionesha kutaka sifa. Na hio ni mbaya kwa muumin, kwasabau inakanusha ikhlas na inabatilisha vitendo ambavyo vimepatikana kwa kujionesha sio kwa ajli ya Allah. Imepokewa na Mahmuod Ibnu Labidi ya kwamba Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) Amesema: [Ni nalo waaogopea juu yenu ni shirki ndogo wakasema ni ipi shirki ndogo?. Akasema: ni Riya. Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) atawaambia wao siku ya kiyama atakapo walipa watu kwa vitendo vyao: Nendeni kwa wale mliyo kuwa mkijionesha katika dunia muangalie mtapata malipo kwao] (Imetolewa na Ahmad).

b. Kukusudia ulimwengu kupitia vitendo vya akhera. Nayo nikufanya baadhi ya vitendo vya akhera kwa ajili ya kupata starehe za ulimwengu. Mfano anae pigana kwa ajili ya kupata mali ya makafiri, au kufundisha ilimu ya sheria kwa sababu ya kupata cheti au kupata kazi. Na hayo kuna hali mbili : (1) Ikiwa kutaka ulimwengu kwa kitendo cha akhera ni chenye kukusudiwa kwa ajili ya ulimwengu, au kikawa ni sawa sawa na kusidio ya akhera. Kufanya hivyo, inapelekea kuharibu ikhlasi, bali inapelekea kupata dhambi, na kubatilisha vitendo vyote. Imetokana na Ubayyu Ibnu Kaab akisema; Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Wape bishara umma huu kumakinika katika miji na kunusurika na kutukuza dini. Mwenye kufanya katika wao kitendo cha akhera kwa ajili ya ulimwengu, hana fungu siku ya akhera]

Ewe Mwenyezi Mungu takasa vitendo vyetu na shirki, utujaalie kuwa na ikhlasi utujaalie ni katika wenye kusikia mema pamoja na kufuata. Na utuepushe na maovu, na utukubalie vitendo vyetu vyote

Khutba ya pili

Shukurani zetu za dhati tuna mshukuru Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) alie mtumiliza Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) ni rehema kwetu sisi alie na huruma mwingi wa sikitiko. Na sala na Salamu zimshukie Mtume wa mwisho wa Mitume. Na Sahaba zake na kila alie wafuata wao kwa wema mpaka siku ya kiyama.

Maudhui yetu ni kukamilisha khutuba ya kwanza nayo ni kujitakasa. Kama tunavyo jua kila mti una mtunda yake. Je matunda ya kujitakasa ni yapi?

Matunda ya Kuvitakasa Vitendo kwa Ajili ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)

Ni kuthibitisha tawhidi na Akida ya Muislamu, pamoja na kusalimika na unafiki.

Kuingia Peponi na kuepukana na moto. Na Muisilamu anapo ingia motoni ni kuwa hana uhakika wa imani.

Kukubaliwa vitendo na kuongezewa malipo.

Kusamehewa madhambi

Kuonja utamu wa ibada na daraja zake.

Kufaulu kupata uombezi wa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) siku ya akhera.

Kupata amani kwa ukamilifu, na uongofu duniani na ahkera.

Kutambua kufaulu na kuufungamanisha moyo na tawfiki.

Kuhifadhiwa na fitna na vitimbi vya shetani.

Kumkomboa mja na ibada ya Shetani

Kufurahiwa na watu na kupendwa.

Kuepushwa moyo wake na uchafu wa kujiona kibri na hasadi.

Kupata nusra ya Mwenyezi Mungu. Na alikuwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) Akijilinda kwa Mwenyezi Mungu kuingia katika shirki kwa sababu ya kukosa ikhlasi.

Anasema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Shirki imefichika kama ubawa wa chungu mweusi nitakujulisha jambo ukilifanya itakuwa kando na wewe shirki ndogo na kubwa. Sema: Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi najilinda kwako na kukushirikisha hali najuwa, naomba msamaha kwako kwa nisilo lijuwa]. Ewe Mwenyezi Mungu turuzuku ikhlasi katika maneno na vitendo.

Mwisho

Enyi Waislamu hakuna katika sisi asiye taka kufaulu. Basi tunapo taka kufaulu tushikamaneni na ikhlasi, kwani ikhlasi ni katika nguzo za kukubaliwa vitendo vyetu. Kama ilivyopokewa kutoka kwa maneno ya wanavyuoni sharuti zakukubaliwa matendo ni mbili: (1) Ikhlasi (2) Kumfuata Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam).

Tunakuomba Mwenyezi Mungu uturuzuku ikhlasi na utuepushe na kujonyesha katika vitendo vyetu. Ewe Mwenyezi Mungu tuhifadhi na shirki zote aina mbili; kubwa na ndogo.





Vitambulisho: