islamkingdomface islamkingdomtwitte islamkingdominstagram islamkingdompinterest islamkingdomtumblr islamkingdomreddit islamkingdomvk


KUOGOPA NA KUMTARAJI NA MWENYEZI MUNGU


8027
wasifu

muislamu anapo fanya matendo mema ni lazima awe na khofu,katika amali ile na kutokubaliwa na allah,na awe na matumaini na kutarajia malipo kwa mola wake ,wala sikufanya ibada bila yakuwa na matarajio yoyote wala kuwa na khofu ya mwenyezi mungu s.w .kuwa na matarajio na kuwa nakhofu ndio msingi wakukubaliwa amali ya mja mbele ya allah

Khutba ya

Himidi zote niza Mwenyezi Mungu Anaefaa kuogopewa na kutarajiwa, hakuna wa kuogopewa na kutarajiwa ila yeye peke yake. Na Swala na Salamu zimshukie Mtume wetu Muhammad (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) pamoja na Jama zake na Swahaba zake wote walio mfuata yeye na kuigiza mwenendo wake.

Nini kuogopa? Na nini kutaraji?

Kuogopa ni tafsiri ya kuuma moyo na kuchomeka kwa sababu ya kuingia katika jambo la karaha, la kuchukiza. Mfano; mtu akafanya kosa mbele ya mfalme kisha likamchukia moyoni kwake kwa kuogopa kufa na ikawa anajua kuwa inafaa kusamehewa na muogopaji zaidi ni yule anayeiogopa nafsi yake. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) Amesema: “Mimi namjua zaidi Mwenyezi Mungu na nina mwogopa zaidi kuliko nyinyi”. Kuogopa na kutaraji ni mbawa mbili wanarukia wenye kujikuribisha na kila jambo nzuri na ni kipando wanakaa kwa hizo njia mbili.

Ewe waja wa Mwenyezi Mungu hakika vitendo vya moyo ni katika jambo kubwa na katika matukufu. Thawabu zake ni tukufu na ni kubwa na adhabu yake ni kubwa na vitendo vya viungo vinafuata vitendo vya moyo na vinajengwa juu yake. Kwa hivyo, ndiyo kukasemwa: Moyo ni mfalme wa viungo na baki ya viungo ni vijakazi wake.

Imepokewa na Anas radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie, akipokea kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) Amesema: [Hawi na msimamo mja mpaka awe na msimamo na moyo wake] (Imepokewa na Ahmad). Maana ya msimamo wa moyo ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu, kumtukuza, kumpenda, kumuogopa, kumtaraji, kupenda twaa yake na kuchukia maasi yake.

Amepokea Muslim kutoka kwa Abu Hurayra Amesema; Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Hakika Mwenyezi Mungu haangalii sura zenu na mali yenu. Lakini ataangalia ndani ya nyoyo zenu na vitendo vyenu].

Amesema Al-Hassan kumuambia mtu: ‘Ufanyie dawa moyo wako, hakika haja ya Mwenyezi Mungu kwa waja ni kutengea nyoyo zao. Na hakika vitendo vya nyoyo ambazo zinapelekea vitendo vizuri na huvutia nyumba ya akhera, na hukemea vitendo vibaya na hupa mgongo ulimwengu na huchukia nafsi mbaya illiyoaswi ni kuogopa na kutaraji.

Na makusudio ya kuogopa ni kupiga moyo na kubabaika na kuogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu. Kwa kutofanya mambo ya haramu au kuacha jambo la wajibu au kuwa na kasoro katika mambo mazuri. Vilevile, ni katika kuogopa kuwa na hamu ya kutokubali Mwenyezi Mungu vitendo vyako, ikatetemeka nafsi na mambo ya haramu na kukimbilia mambo ya kheri. Amesema Ibnul-Qayyim Mwenyezi Mungu amrehemu : ‘Kuogopa ni kwa Waislamu wote na kicho ni kwa wanavyuoni wanaojua ‘.

Enyi Waja wa Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu Amemuahidi mwenye kumuogopa yeye, kumzuia yeye na matamanio na kumsaidia katika Twaa na kumlipa malipo bora. Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى): وَلِمَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ جَنَّتَانِ 46فَبِأَيِّ آَلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَان47ذَوَاتَا أَفْنَانٍ

{{Yule anaemuogopa mola wake atapata mabustani mawili. Ni yapi katika neema za Mwenyezi Mungu munakanusha? mabustani yenye miti yenye matawi mengi}} [Arahmaan : 46 - 48].

Tuangalie watu wema namna walivyokua wakimuogopa Mwenyezi Mungu na kumtarajia. Ilikua kuogopa kwao ni hali ya juu wakifanya vitendo vizuri na kutaraji rehma ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, kuogopa iliwatengeneza na wakasafisha vitendo vyao na yakawa mazuri maregeo yao. Amesema Abu Hafsi: ‘Kuogopa ni kibati cha Mwenyezi Mungu huwanyosha waliokimbia mlango wake’. Na akasema : ‘kuogopa ni taa katika moyo’.

Nakumuogopa Mwenyezi Mungu inapelekea kufanya mambo ya akhera na ni ngome ya kila jambo. Inamsukuma mja kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu na malipo yake. Inapelekea kuwa na hima ya juu kufanya vitendo vizuri.

Kumuogopa Mwenyezi Mungu huzuia nafsi na shahwa zake na huikemea na upotevu na inamuhami kumpelekea kwa kila jambo zuri na kufaulu. Na kumuogopa Mwenyezi Mungu ni sehemu katika sehemu za kumpwekesha Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, inafaa iwe kuogopa kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu ni sehemu katika sehemu ya shirki kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Na ameamrisha Mwenyezi Mungu kumuogopa yeye katika Aya nyingi na akakataza kumuogopa asiyekuwa yeye. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)::

فقال تعالى) : إِنَّمَا ذَلِكُمُ الشَّيْطَانُ يُخَوِّفُ أَوْلِيَاءَهُ فَلَا تَخَافُوهُمْ وَخَافُونِ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ )[آل عمران: 175]

{{Hakika huyo shetani ambaye anawafanya uwoga marafiki wa Mwenyezi Mungu musimuogopeni yeye niogopeni mimi ikwa nyinyi ni waumini wa kweli, mukiwa Waislamu wa kweli}} [Al-Imran : 175].

Na katika Hadithi za Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Imepokewa na Anas radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie Amesema: Alikuja Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) Akasema: “ Lau mgejua ninayo yajua mgalicheka kidogo na mkalia kwa wingi”. Masahaba wakajifunika nyuso zao wakatoa koromo za kilio”. (imepokewa na Bukhari na Muslim).

Khutba ya pili

Himidi na sifa njema zisizo kifani zisizo na shaka ni za Mwenyezi Mungu Ambaye hakuzaa wala hakuzaliwa, Anayefaa kuogopwa na kutarajiwa Yeye pekee. Na Swala na Salamu zimshukie Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam).

Maudhui ni kubainisha uhakika wa kutaraji nao; ni kuwa na tamaa katika kupata malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na kuogopa inayopendeza ni ile inayo kuvutia kufanya vitendo vyema na ina kuzuiya kufanya ya haramu. Na pindi uoga unapopita kiasi unapelekea kukata tamaa na rehma ya Mwenyezi Mungu na hilo ni katika madhambi makubwa.

Amesema Ibnu Rajab Amrehemu yeye Mwenyezi Mungu: ‘Kiasi kinacho faa kutokana na kuogopa ni iliyo msaidia mtu kutekeleza jambo la lazima na kujiepusha na mambo ya haramu. na ikiwa juu hapo; nao ni kupelekea nafsi kufanya bidii kufanya Twaa ya ziada na kujizuia na yenye kuchukiza na kukunjua itakuwa ni yenye kupendeza. Na ikizidi juu ya hapo linarithisha magonjwa au kufa kwa moyo. Na kusababisha nafsi kukataa kukimbilia vitendo vizuri na hili si jambo lakupendeza.

Baada ya hapo tuangalie kutaraji nayo ni kuwa na tama kwa malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu ya kufanya vitendo vyema. Na sharti ya kutaraji ni kutanguliza vitendo vizuri na kujizuia na mambo ya haramu. Ama kuacha ya wajibu na kufuata matamanio na kutamani malipo kwa Mwenyezi Mungu na kumtarajia yeye, hapo itakua ni kutaka amani na adhabu ya Mwenyezi Mungu na wala si kutaraji. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى: (أفَأَمِنُوا مَكْرَ اللَّهِ فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللَّهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْخَاسِرُونَ) [الأعراف: 99]:.

{{Hawaaminishi adhabu ya Mwenyezi Mungu ila watu waliopata hasara}} [Al-Araaf:99]. Enyi Waislamu: Jueni ya kwamba kutaraji bila vitendo ni kujidanganya. Na Mwenyezi Mungu amekataza Hilo. Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) : يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّ وَعْدَ اللَّهِ حَقٌّ فَلَا تَغُرَّنَّكُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَلَا يَغُرَّنَّكُمْ بِاللَّهِ الْغَرُورُ) [فاطر: 5]

{{Enyi watu hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, basi yasiwadanganye maisha ya kilimwengu wala Yule mdanganyaji mkubwa (Iblis) na sikudanganyeni juu ya Mwenyezi Mungu}} [Fatir: 5].

Mwisho

Ndugu Waislamu tumuogope Mwenyezi Mungu na tutarajie kheri kutoka kwake. Natuogope adhabu yake ili tupate malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu malipo ya akhera na dunia. Mwenyezi Mungu atujalie ni wenye kumuogopa yeye na kumtarajia yeye, na atupe kheri ya dunia na akhera atujalie ni katika wenye kusikia mema na kuyafuata, na mabaya tuyaepuke.





Vitambulisho: