islamkingdomface islamkingdomtwitte islamkingdominstagram islamkingdompinterest islamkingdomtumblr islamkingdomreddit islamkingdomvk


athari ya kusuhubiana na rafiki mwema


5521
wasifu
Rafiki ana mchango mkubwa wakuweza kumuathiri kwa yule alie suhubiana na yeye ima kwa kheri ama kwa shari,na ukitaka kumjua mtu muangalie alie suhubiana na ye,ikiwa rafiki yake ni mwema basi na yeye atakuwa ni mwema,na ikiwa rafiki yake ni muovu basi na yeye ni kadhalika.kwa hivyo dini yetu imetuamrisha tusuhubiane na marafiki wema,na kututahadharisha na marafiki wabaya.
Khutba ya

Mwanadamu hawezi kuishi peke yake ana haja ya usaidizi na kutangamana na watu wengine. Kwa ajili hiyo uislamu umekuja kuitikia mwito wa maumbile, uislamu ukaweka ibada ambazo zinafanywa na watu wengi kwa pamoja mfano wake Swala. Uislamu ni dini ya maumbile, ushahidi wa hayo ni Hadithi iliyopokewa na Abu Hureira: “ Yoyote anayezaliwa huzaliwa katika uislamu isipokuwa wazazi wake humfanya mtoto wao kuwa myahudi au mnaswara au majusi”. Kama Mwenyezi Mungu alipomuumba Adam na Hawaa ili waishi pamoja wala hakumuacha peke yake amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال الله تعالى) : هُوَ الَّذِي خَلَقَكُمْ مِنْ نَفْسٍ وَاحِدَةٍ وَجَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا لِيَسْكُنَ إِلَيْهَا) [الأعراف: 189]

{{Yeye ndiye aliyekuumbeni katika nafsi moja; na katika nafsi hiyo ameumba wake wao ili mpate utulivu kwake}}. Uislamu umetiliwa nguvu kutokana na sababu nyingi kama kuwekwa ibada za pamoja mfano wake swala ya ijumaa, swala ya jamaa na nyenginezo. Dhihirisho la haya alipoazimia Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) kuchoma nyumba za wasio kuja kuswali swala za jamaa. Na dharura kwa uhai ni kuchagua mtu anayesuhubiana nae ili amkumbushe anaposahau na kumjuza anapokuwa mjinga, amesema mshairi wa kiarabu: “ Mja usimuulize bali muangalie rafiki yake kila rafiki kutokana na marafiki huongozana. Akiwa rafiki huyo ni muovu jiepusheni nae kwa haraka, na ikiwa ni mwema husuhubiana nae utaongoka”.

Uchaguzi wa rafiki mwema umejengwa kutokana na msingi wa kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake na dini yake. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال الله تعالى) : إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللَّهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آَمَنُوا الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ) [المائدة: 55]

.

{{Hakika rafiki yenu khasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walioamini ambao husimamisha sala na hutoa zaka, na hali wakiwa wananyenyekea. Na atekayefanya urafiki na Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walioamini. Kwani kundi la Mwenyezi Mungu ndio litakalo shinda}}. Na katika matunda ya imani ni kuchagua rafiki mwema. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

ويقول: (لَا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآَخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آَبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ) [المجادلة: 22]

{{Huwapati watu wanaomuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, kuwa wanawapenda wale wanaompinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake}}. Na kemeo kubwa ni kuwapenda maadui wa Mwenyezi Mungu.

Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

وقوله تعالى: (مُحَمَّدٌ رَسُولُ اللَّهِ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ) [الفتح: 29] {{Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye ni wenye nyoyo thabiti mbele ya makafiri na wenye kuhurumiana wao kwa wao}}.

Na akasema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

وقوله تعالى: (يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا مَنْ يَرْتَدَّ مِنْكُمْ عَنْ دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ) [المائدة: 54]

{{Enyi mlioamini, Atakayeiacha miongoni mwenu dini yake, basi hivi karibuni Mwenyezi Mungu ataleta watu ambao atawapenda, nao watampenda, wanyenyekevu kwa Waislamu wenzao, wenye nguvu juu ya makafiri}}.

Mwenye akili siku zote huwakimbia marafiki waovu kama anavyo mkimbia mtu Simba, tazama Neno lake Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قوله تعالى): وَيَوْمَ يَعَضُّ الظَّالِمُ عَلَى يَدَيْهِ يَقُولُ يَا لَيْتَنِي اتَّخَذْتُ مَعَ الرَّسُولِ سَبِيلًا 27 يَا وَيْلَتَى لَيْتَنِي لَمْ أَتَّخِذْ فُلَانًا خَلِيلًا28 لَقَدْ أَضَلَّنِي عَنِ الذِّكْرِ بَعْدَ إِذْ جَاءَنِي وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِلْإِنْسَانِ خَذُولًا) [الفرقان: 29]

{{Na siku dhalimu atajiuma mikono yake vidole vyake na huku akisema: Laiti ningalishika njia ya haki nikawa pamoja na Mtume}}. Dhalimu aliyekusudiwa katika Aya iliyotangulia ni ‘Uqbatu ibn Abi Mu’ayit na aliyempoteza katika uongofu Ummayah ibn Khalaf.

Amefananisha Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) rafiki mwema na rafiki muovu kama mfano wa anayebeba miski na mwenye kufua vyuma kwa anae beba miski ima atakuuzia ima utapata kutoka kwake harufu mzuri na mfua vyuma ima atachoma nguo zako au utapata harufu mbaya]. Je hauoni neno la Luqman juu ya mtoto wake: Ewe mwanangu tangamana na wanavyuoni hakika Mwenyezi Mungu hukuhuisha nyoyo kwa nuru ya hikima, kama anavyohuisha ardhi iliyokufa.”

Khutba ya pili

Matunda ya kusuhubiana na rafiki mwema kuongoka kwa mtu mmoja ni kuongoka kwa jamii na kuongoka kwa jamii ndio sababu ya kupata baraka inayotoka mbinguni na ardhini. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) : وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَى آَمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِمْ بَرَكَاتٍ مِنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ وَلَكِنْ كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ) [الأعراف: 96]

{{Na lau kama watu wa miji wangaliamini na kuogopa, kwa yakini tungaliwafungulia baraka za mbingu na ardhi. Lakini walikadhibisha; tukawapatiliza kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma}}. Watu wa peponi wote ni marafiki wema.

Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى: (إِنَّ الَّذِينَ آَمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَانَتْ لَهُمْ جَنَّاتُ الْفِرْدَوْسِ نُزُلًا ) [الكهف: 107]

{{Kwa yakini walioamini na kufanya vitendo vizuri, makazi yao yatakuwa hizo za Firdaws}}.

Na Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) :

وقوله تعالى: (وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِمْ مِنْ غِلٍّ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ) [الأعراف: 43] {{Na tutaiondoa bughudha vifuani mwao (wawe wanapendana wote kweli kweli) mbele yao iwe inapita mito}}. Wema waliotangulia ni mfano bora wa kusuhubiana. Pindi Salman alipomtembelea Abu Dardai akamuona Mama Dardai nae akamuuliza kuhusu Abu Dardai nae akamjibu kuwa ametoka na muda si mrefu atarudi. Ummu Dardai akamjulisha Salman tabia ya Abu Dardai ya kuachana na dunia na kutoangalia watu wake. Pindi aliporudi Abu Dardai mazungumzo yao yalikuwa kama hivi ifuatavyo:

Abu Dardai alimwambia Salama: Kula chakula hichi mimi nimefunga. Salman akajibu sili chakula hichi mpaka ule wewe. Abu Dardai akala chakula hicho. Ilipofika usiku Abu Dardai alitaka kusimama (Qiyamulail). Salman akamwambia: lala. Abu Dardai akalala, jambo hilo likaendelea mara mbili tatu ilipofika usiku wa mwisho Salman akasema: amka sasa Mola wako na nafsi yako pia ina haki kwako. Vile vile pia mke wako ana haki kwako, ipe kila haki haki yake. Aliposikia Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akasema: “ Amesema kweli Salman.” Tazama vipi waja wema wanavyosaidiana kwa amali njema na kumcha Mwenyezi Mungu.

Mfano wa rafiki muovu na mwisho wake, Abu Talib alipokuwa anafikiwa na mauti Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) alimtembelea na hapo alikuwepo Abu Jahal na ‘Abdallah Ibn Abi Umaya Ibn Mughaira. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akasema kumuambia Abu Talib aseme “Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu “ neno ambalo litakutolea hoja mbele ya Mwenyezi Mungu, akasema Abu Jahal na ‘Abdillah Ibn Abi Ummayah unaipa nyongo mila ya AbdulMutwalib. Hakuacha Mtume wa Mwenyezi Mungu kumkariria, na wao pia wakikariri “Unaipa nyongo mila ya AbdulMutwalib” mwishowe akasema yeye yuko katika mila ya AbdulMutwalib.

Enyi baba zangu nyote ni wachunga na kila mmoja ataulizwa kwa kile anacho kichunga. Itakuwa ni khiana baba kuwaacha watoto wake bila ya kuwauliza wanakwenda wapi, hali ya siku hizi hawaulizi wanapokwenda au walikuwa pamoja na nani? Na wapi wamelala? Wala hajui baba kwamba mtoto wake alikuwa na rafiki wa kishetani wakimuharibu dini, akili yake na uislamu wake. Tahadhari na marafiki waovu, na ni juu ya barobaro kuchagua rafiki mwema ambao watakaomsaidia katika haki na kumjuza.

Mwisho

Ndugu katika Imani, ni muhimu sana kuchagua rafiki mwema ambaye atakusaidia katika kufanya mambo ya kheri. Pindi unapo sahau anakukumbusha na ukikosea anakunasihi kwa njia mzuri.

Ewe Mwenyezi Mungu turuzuku rafiki wema na utuepushie na rafiki waovu, uturuzuku rafiki wema ambao watatusaidia katika kukushukuru na kukutaja na kukuabudu na uturuzuku kusuhubiana na Mtume wako.

Vitambulisho: