islamkingdomface islamkingdomtwitte islamkingdominstagram islamkingdompinterest islamkingdomtumblr islamkingdomreddit islamkingdomvk


BAADA YA MAUTI


14733
wasifu
ndugu yangu kuna suali muhimu sana kwa kila moja wetu ajiulize je! baada yakifo waenda wapi.? hili ni suala yatakika kila muislamu aliweke akili mwake,kwa sababu siku ya kiyama hakuna sehemu ya mtu atakapo enda ima ni peponi ama ni motoni kwa hivyo nitufanye amali njema zitakazo tufaa siku ya kiyama.
Khutba ya

Baada ya kumshukuru na kumhimidi Mwenyezi Mungu na kumswalia Mtume wetu Muhammad. Nawausia pamoja na kujiusia nafsi yangu juu ya kumcha Mwenyezi Mungu na kufuata nyayo za Mtume Muhammad na mwendo wa Masahaba zake na Watu wema.

Nini kufa? Kufa ni kuepukana roho na kiwiliwili, au kufa ni kukatika matumizi ya roho kwa kiwiliwili na kukosa kiwiliwili ala yake na kumuepusha mtu na amali yake na watoto wake na mke wake. Kufa inakata utamu wa maisha ya kilimwengu na kwenda ulimwengu mwengine. Mtu ambae alikuwa akifurahia maisha ya ulimwengu amepata khasara baada ya kufa. Na yule ambae alikuwa akifurahi kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu basi atapata neema kubwa na ina kamilika kufaulu kwake.

Watu wengi hudhania ya kwamba Mtu anapo kufa na akazikwa amemaliza kila kitu na amepumzika na ulimwengu, wala halimjii yeye jambo lolote. Kudhania hivyo ni kosa kubwa bali hakika Mwanadamu baada ya kufa kwake anaingia katika maisha mapya, maisha ya barzakh na kutoka maisha ya barzakh huenda kwenye maisha ya Akhera ambayo ndiyo maisha ya mwisho na ya milele.

Njooni Waja wa Mwenyezi Mungu tuangalieni kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) zina semaje kujibu suala; Ni nini baada ya kufa ?

Hakika Qu’rani imebainisha wazi na Hadithi za Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) yatakayo tokea baada ya kufa. Wakati anapokufa Mwanadamu na akazikwa, jambo la kwanza linalompata ni fitina ya kaburi.

Imepokewa katika sahihi mbili ya Bukhari na Muslim kutoka kwa Anas Bin Malik Akipokea kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Hakika mja anapo wekwa katika kaburi lake na wakaondoka watu wake, Anasikia mlio wa viatu vyao. Akasema wanamjia Malaika wawili wakamkalisha wakamuambia unasemaje juu ya mtu huyu. Akasema: Ama Muislamu atasema: Nilikuwa nikishuhudia ya kwamba ni mja wa Mwenyezi Mungu na ni Mtume wake. Akasema: Ataambiwa angalia makao yako motoni umebadilishiwa pepo. Akasema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) Atayaona makao mawili. Amesema Qatada tumeelezwa: hukunjuliwa kaburi lake dhiraa sabiini na atajaziwa kila aina ya chakula. Ama aliye kufuru na mnafiki ataulizwa unajua nini juu ya Mtu huyu atasema sijui nilikuwa nikisema walivyokuwa wakisema watu ataambiwa hukujuwa na wala hukusoma atapigwa nyundo ya chuma moja moja, watasikia watu wote wasiokuwa viumbe aina mbili (wanadamu na majini)].

Na imepokewa na Abu Ayyub radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie Amesema : [ Alitoka Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) na jua limetoka, Akasikia sauti ya Yahudi ana adhibiwa katika kaburi lake’ (Bukhari na Muslim). Kwa hivyo, Alikuwa Mtume haswali swala yeyote ila alikuwa akijilinda na adhabu ya kaburi. Na akaamrisha hivyo watu wake].

Kisha ataadhibiwa kafiri na mnafiki. Na Mu’mini atastarehe. Basi tujiulize nafsi zetu, je tumeandaa jawabu ya masuali ya kaburini. Ewe mja wa Mwenyezi Mungu, hakika hiko ni kiyama kitakuja hakina shaka. Na baada yayote atawafufuwa Mwenyezi Mungu walioko kwenye makaburi. Na dalili ni Aya tukufu:

قال تعالى) : أَوَلَمْ يَرَ الْإِنْسَانُ أَنَّا خَلَقْنَاهُ مِنْ نُطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُبِينٌ 77وَضَرَبَ لَنَا مَثَلًا وَنَسِيَ خَلْقَهُ قَالَ مَنْ يُحْيِي الْعِظَامَ وَهِيَ رَمِيمٌ 78قُلْ يُحْيِيهَا الَّذِي أَنْشَأَهَا أَوَّلَ مَرَّةٍ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَلِيمٌ79) [يس77: 79]

{{Je hatambui Mwanadamu ya kwamba tumemuumba kwa tone la manii? mara amekuwa hasimu yetu aliye dhahiri. Na akatupigia sisi mfano, na akasahau kuumbwa kwake. Akasema ni nani atakayeihuisha mifupa na hali imesagika?. Sema Ewe Muhammad; Ataihuisha Yule aliyeiumba mara ya kwanza na yeye ni mjuzi wa kila namna ya kuumba}} [Yaasin : 77 – 79]. Halafu atawakusanya watu wote kwa ajili ya hisabu. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

وقال : (وَنَحْشُرُهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَى وُجُوهِهِمْ عُمْيًا وَبُكْمًا وَصُمًّا مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ كُلَّمَا خَبَتْ زِدْنَاهُمْ سَعِيرًا) [الإسراء: 97]

{{Na tuwakusanya siku ya kiama hali kuwa wanakokotwa juu ya nyuso zao na hali ya kuwa ni mapofu na mabubu na viziwi. Makazo yao ni Jahannamu. Kila ukifanya kusinzia kidogo tutawazidishia mwako}} [Israai : 97].

Haya ndiyo matukio ya kuogopesha utawaona wabaya na madhalimu na wana fiki wameinamisha vichwa vyao, hawarudishi macho yao, wala hasemi siku hiyo ila aliye pewa ruhusa na Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Na nyoyo siku hiyo zimefika kooni wamekasirika na madhalimu hawana muombezi wala rafiki mwenye kutiiwa. Na siku hii kiasi chake ni miaka khamsini alfu.

Waja wa Mwenyezi Mungu, wakati huo watu watasimama mbele ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala), hakuna pa kufichika. Siku hiyo watu watatoka makaburini vikundi vikundi kwa ajili ya kuona vitendo vyao. Na itaanza hisabu. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Ataletwa kafiri siku ya kiama aambiwe waonaje lau ungekuwa na mjazo wa ardhi dhahabu ungalijikomboa? atasema ndiyo. Ataambiwa umeulizwa ambalo ni sahali kuliko hilo]. Na katika mapokezi mengine: [Nimekuuliza ambalo ni sahali kuliko hili na wewe uko katika mgongo wa Adam usimshirikishe Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) ukakataa na ukanishirikisha na viumbe vingine].

Enyi waisilamu haya ni baadhi ya yale yatakayo tokea siku ya kiama, mbali na yale tuliyo ghafilika nayo. Na kila mmoja katika sisi atakuwa juu ya yale aliyo yafanya katika maasi. Ewe hakimu, Ewe rais, utatubiya lini? rudi kwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Utamwambia nini Mola wako. Je hukumbuki neno la Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) : [ Hakuna mchungaji yoyote aliye pewa uchungaji na Mwenyezi Mungu, atakufa siku atakayo kufa na yeye ni mdanganyifu ila ataingiya motoni].

Enyi mawaziri na manaibu hamuogopi Mwenyezi Mungu kwa mliyoyabeba juu ya mabega yenu. Je mume jiandaa vipi na hali hii ya utisho miongoni mwa fitina ya kaburi na adhabu yake kukusanywa kwa ajili ya hisabu. Nini mume jianda na siku hiyo. Ewe Mwenye kufanya khiyana, Je utawacha lini khiyana zako, utasimamisha lini swala. Rudi kwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Na wewe mwizi utaaacha lini wizi wako kwa hakika huna budi lazima upitie njia hii ngumu. Na wewe barobaro umejiandaa vipi na siku hii. Je umejiandaa na siku ya kufa. Na wewe msichana wadhani ya kwamba kifo hakitakuja kwako?

Na baada ya hapo zifunguliwe vitabu. Na wenye kupewa vitabu ni aina mbili; ni mwenye kupokea kitabu kwa mkono wa kulia, na mwenye kupewa kitabu kwa mkono wa kushoto. Kisha iwekwe mizani kwa uadilifu siku ya kiama. Baada ya hayo itakuja sirat na kila mmoja atapitia njiya hiyo. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) atuafikie tuweze kufaulu katika siku hii nzito.

Khutba ya pili

Baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) na kumsalia Mtume Muhammad na Sahaba zake. Maudhui ni kubainisha hakika nyumba za akhera ni mbili; ima ni pepo au ni moto. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى (وَكَذَلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ قُرْآَنًا عَرَبِيًّا لِتُنْذِرَ أُمَّ الْقُرَى وَمَنْ حَوْلَهَا وَتُنْذِرَ يَوْمَ الْجَمْعِ لَا رَيْبَ فِيهِ فَرِيقٌ فِي الْجَنَّةِ وَفَرِيقٌ فِي السَّعِيرِ )[الشورى: 7]

{{Na namna hivi tuliwafunulia Qur’an kwa lugha kiarabu ili uwaonye watu wa Makka na walio katika vijiji na uwakhofishe siku ya mkusanyiko ambayo haina shaka na kundi moja litaingia peponi na kundi moja motoni}} [Ashuraa : 7].

وقال) : إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآَيَةً لِمَنْ خَافَ عَذَابَ الْآَخِرَةِ ذَلِكَ يَوْمٌ مَجْمُوعٌ لَهُ النَّاسُ وَذَلِكَ يَوْمٌ مَشْهُودٌ) [هود: 103].

{{Hakika katika hilo kuna mazingatio kwa Yule anayeogopa adhabu ya Akhera. Hiyo ndio siku itakayokusanywa watu na hiyo ni siku itakayoshuhudiwa}} [ Huud :103]. Na Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

 

وقال : (وَسِيقَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِلَى جَهَنَّمَ زُمَرًا حَتَّى إِذَا جَاءُوهَا فُتِحَتْ أَبْوَابُهَا وَقَالَ لَهُمْ خَزَنَتُهَا أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِنْكُمْ يَتْلُونَ عَلَيْكُمْ آَيَاتِ رَبِّكُمْ وَيُنْذِرُونَكُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَذَا قَالُوا بَلَى وَلَكِنْ حَقَّتْ كَلِمَةُ الْعَذَابِ عَلَى الْكَافِرِينَ 71قِيلَ ادْخُلُوا أَبْوَابَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا فَبِئْسَ مَثْوَى الْمُتَكَبِّرِينَ72 وَسِيقَ الَّذِينَ اتَّقَوْا رَبَّهُمْ إِلَى الْجَنَّةِ زُمَرًا حَتَّى إِذَا جَاءُوهَا وَفُتِحَتْ أَبْوَابُهَا وَقَالَ لَهُمْ خَزَنَتُهَا سَلَامٌ عَلَيْكُمْ طِبْتُمْ فَادْخُلُوهَا خَالِدِينَ 73) [الزمر71: 73]

{{Na waliyo kufuru watapelekwa katika moto makundi makundi, mpaka watakapoifikia itafunguliwa milango yake}} [Azzumar : 71].

Enyi waja wa Mwenyezi Mungu, fanyeni haraka kurudi kwa Mwenyezi Mungu na mufanye vitendo vizuri kwa kuchukua zawadi za Akhera. Muogopeni Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) waja wa Mwenyezi Mungu, na mjue ya kwamba mtukufu wenu ni amchae Mungu. Na ambae amemchelewesha na vitendo vyake hakimsaidii kizazi chake na hakika hayo ni vitendo vyenu mlivyo vichuma. Atakaye pata kheri na amshukuru Mwenyezi Mungu, na mwenye kupata kinyume ya hayo na asilaumu isipokuwa nafsi yake.

Mwisho

Tumuogopeni Mwenyezi Mungu na tujiandae na kifo, na yatakayotokea baada ya kufa. Kwani hakuna budi kila kinacho ishi ulimwenguni kitakumbana na kifo hakuna mnyama wala binadamu, wote watakumbana na kifo na baadae kukutana na Mola wao na kulipwa kila moja kwa aliyofanya.

Mwenyezi Mungu Atujaalie ni katika wenye kujiandaa na kifo na atupe mwisho mwema katika vifo vyetu. Atujaaliye ni katika wenye kusikia mema pamoja na kuyafuata, na kujiepusha na mabaya.





Vitambulisho: