islamkingdomface islamkingdomtwitte islamkingdominstagram islamkingdompinterest islamkingdomtumblr islamkingdomreddit islamkingdomvk


Iddi ya Fitri


6577
wasifu
Idul-Fitri ni neema, furaha, ibada, na kikamilisho cha mwezi wa Ramadhani tukufu. Katika Idi hii kuna Zaka za Fitri ambazo zitamsafisha mwenye kufunga na upuzi na uchafu . Katika hii Idi itajitokeza maana mengi ya Uislamu ya Kijamii na Kibinadamu. Katika Idi nyoyo zinakuribiana juu ya mapenzi na watu wanakusanyika baada ya kupambanukana. Katika Idi kuna kukumbusha watu haki ya wanyonge katika jamii ya Kislamu, mpaka furaha ienee kila kila nyumba na neema iingie kila familial.
Khutba ya

Iddi ya Fitri ni Iddi ya kwanza kwa Waislamu. Waislamu wanasherehekea katika mwezi wa Shawwal kinyume na Iddul adhha ambapo Waislamu wanasherehekea katika mwezi wa Dhulhijjah. Waislamu wanakula baada ya kufunga mwezi mzima, ni haramu kufunga siku hiyo. Na muda wa kusherehekea ni siku moja hadi siku sita.

Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) kukamilisha kufunga mwezi wa Ramadhani. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى): شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآَنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ فَمَنْ شَهِدَ مِنْكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَنْ كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِنْ أَيَّامٍ أُخَرَ يُرِيدُ اللَّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّهَ عَلَى مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ )[البقرة: 185]

 

{{Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa katika mwezi huo Qur’an ili iwe uongozi kwa watu na hoja zilizo wazi wa uongozi na upambanuzi (wa baina ya haki na batili).

Atakayekuwa katika mji katika huu mwezi wa Ramadhani afunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu ya siku alizoacha kufunga katika siku nyingine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mapesi wala hakutakieni yalio mazito, na pia anakutakieni mtimize hesabu hiyo, na anakutakieni kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongozeni, ili mpate kushukuru}}. Amesema ‘Umar siku mbili hizi Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amekataa kufunga yaani Iddul-fitr (baada ya mwezi wa Ramadhani) na Idul-Adhha (Baada ya Hajj).

Amepokea Anas kwamba Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) alikwenda Madina na walikuwa wana siku mbili za kucheza, Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akasema {Mwenyezi Mungu amekubadilishieni siku mbili hizo kwa Iddul-fitr na Iddul Adhha].

Siku ya Iddi ni siku ya mapambo. Imepokewa kwa Ibnu ‘Umar kuwa alinunua juba sokoni akamuuzia Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) kuwa ajipambe nalo siku ya Iddi, Amepokea Anas Ibnu Malik kuwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [Haendi kuswali swala ya Iddul-fitr mpaka ale Tende].

Hukumu ya Utoaji wa Sadaka ya Fitri

Amepokea Ibnu ‘Abbas kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amefaradhisha Zakatul-fitri kumtakasa aliyefunga kutokana na michezo, pia kuwa ni chakula cha maskini. Mwenye kutoa kabla ya swala basi ametoa zaka na atakayetoa baada ya swala basi hio ni sadaka miongoni mwa sadaka.

Kupiga Takbir za Iddi

Asili ya jambo hilo Neno lake Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) :

قال الله تعالى : (وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّهَ عَلَى مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ) [البقرة: 185]

{{Anakutakieni mtimize hisabu hiyo, na anakutakieni kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongozeni, ili mpate kushukuru}}.

Imepokewa na Ibnu ‘Umar akisema kuwa: [Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) alikuwa akipiga Takbiri alipo kwenda kuswali swala ya Iddi].

Khutba ya pili

Namna ya kuswali Swala ya Iddi

Imethibiti kwa Ibn ‘Abbas kuwa ameswali swala ya Idd pmoja na Mtume na Abubakar pamoja na ‘Umar na ‘Uthman kuwa wote wameswali kabla ya khutba. Amesema Ibnu Abbas kuwa Mtume ameswali Idd kwa rakaa mbili na hakuswali kabla ya hapo au baada ya hapo.

Ziara Baada ya Swala na kupeana Zawadi

Imethibiti Hadithi kutoka kwa Ibnu ‘Abbas kuwa ametoka pamoja na Mtume siku ya Iddul-fitr na Iddul-Adhha wakaswali kisha aka khutubu Mtume na akawatembelea wanawake na kuwapatia mawaidha na akawaamrisha kupeana sadaka. Abubakar aliingia nyumba Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) na ‘Aisha alikuwa na vijakazi viwili wakipiga matwari. Akawakataza Abubakar. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akasema: [ Waache kwani kila jami ina Iddi yao].

Kufunga Siku sita za Shawwal.

Amesema Abu Ayub Answar kuwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema [ Atakayefunga Ramadhani kisha akafuatilizia siku sita za Shawaal ni kama aliyefunga mwaka mzima].

Amesema Hasan Al-Basri kuwa Mwenyezi Mungu ameridhia kufunga siku sita za Shawwal na ufungaji wa mwaka mzima.

Kumshukuru Mwenyezi Mungu katika Siku za Iddi

Amesema Mwenyezi Mungu ( Subhaanahu wa Taala):

قوله تعالى) : وَاشْكُرُوا لِي وَلَا تَكْفُرُونِ) [البقرة: 152]

{{Na mnishukuru Mimi na wala msikanushe}}.

Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى: (وَإِذْ تَأَذَّنَ رَبُّكُمْ لَئِنْ شَكَرْتُمْ لَأَزِيدَنَّكُمْ وَلَئِنْ كَفَرْتُمْ إِنَّ عَذَابِي لَشَدِيدٌ ) [إبراهيم: 7]

{{Na kumbukeni alipotangaza Mola wenu : kama mkishukuru, nitakuzidishieni; na kama mkikufuru, jueni kuwa adhabu Yangu ni kali sana}}.

Amesema ‘Imran Ibn Huswain kuwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema kuwa Mwenyezi Mungu amesema: [ Mwenyezi Mungu akimneemesha mja hupenda kuona athari ya neema hiyo kwa mja wake]. Kwahivyo, ndugu Waislamu dhihirisheni neema za Allah (Subhaanahu wa Taala) kwa kuwasaidia maskini katika siku hii muhimu siku ya furaha.

Mwisho

Lengo la kufunga ni kumcha Mwenyezi Mungu kama alivyosema Mwenyezi Mungu. Na maana ya kumcha Mwenyezi Mungu ni kufuata maamrisho yake yote na kuachana na makatazo yote aliyo kataza. Kudumu na msimamo wa uchaji Mungu paka kufikiwa na mauti.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atupe Taqwa, na atupe maghfira, rehema na kuwachwa huru na moto wa Jahannam.

Vitambulisho: