islamkingdomface islamkingdomtwitte islamkingdominstagram islamkingdompinterest islamkingdomtumblr islamkingdomreddit islamkingdomvk


UJIRANI NA HAKI ZAKE KATIKA DINI YA UISLAMU


11331
wasifu
Uislamu umeusia juu ya jirani na kumpa cheo kikubwa. Jirani katika Uislamu ana heshima yenye kutunzwa na haki nyingi ambazo hazukwa zinajulikana na kanuni na sheria za kibinadamu na nchi. Kanuni na sheria zinazompuuza jirani na na kufurahia kumvunjia heshima yake. Na miongoni mwa haki kubwa za jirani ni kuwa Jibrili, amani imshukie, aliendelea kumuusia Mtume, rehema na amani zimshukie, mpaka akadhani kuwa atamrithisha.
Khutba ya

Ndugu zangu Waislamu, kila mmoja anahitaji mazungumzo hayo, maongezi ambayo Jibril hakuacha kumuusia Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) kuhusu jirani mpaka akadhani ana haki ya kurithi. Jirani ana haki zinapaswa kulindwa na hizo haki za jirani huyo ni sawa awe Muislamu au kafiri, mwema au muovu, rafiki au adui aliyekuwa karibu au mbali. Na kila mmoja ana daraja kuliko mwingine inazidi au inapungua kutokana na ukaribu wake, dini yake, tabia yake na ukaribu wake. Uislamu umeusia kuhusu jirani na kuhifadhi haki zake ambazo hazijatambuliwa na kanuni. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) وَاعْبُدُوا اللَّهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَبِذِي الْقُرْبَى وَالْيَتَامَى وَالْمَسَاكِينِ وَالْجَارِ ذِي الْقُرْبَى وَالْجَارِ الْجُنُبِ ([النساء: 36] {{Mwabuduni Mwenyezi Mungu wala msishirikishe na chochote. Na wafanyeni ihsani wazazi wawili, na jamaa, na mayatima, na maskini, na jirani walio karibu au jirani walio mbali}}.

Amepokea Ibn ‘Umar, amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Hakuacha Jibril kuniusia kuhusu jirani mpaka nikadhani kuwa jirani atarithi]. Amepokea Abu Huraira hadithi kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akisema: [Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho azungumze mambo ya kheri au anyamaze, na anayemuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho amkirimu jirani yake].

Amesema Sheikh Abu Muhammad: Kuhifadhi haki ya jirani ni katika kukamilika kwa Imani. Na watu katika zama za jahilia walikuwa wakihifadhi haki za jirani na wakiusia kwa kuwafanyia wema mfano kumpa zawadi, kumtolea salamu, kumuonyesha uso wa furaha na kujua hali yake na kumsaidia anacho kihitaji.

Amepokea Abu Huraira: ‘ Haki za Muislamu juu ya Muislamu mwenzake ni sita:-

Kumsalimia anapokutana naye

Kuitikia mwito anapokuita

Kupokea nasaha anapokuusia

Kumrehemu anapo chemua

Kumtembelea anapokuwa mgonjwa

Kufuata jeneza lake anapo kufa

Tahadhari Kuwaudhi Majirani

Ndugu zangu Waislamu ni haramu kuudhi majirani. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi asiudhi jirani zake]. I

mepokewa na Shureyh amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Naapa kwa Mwenyezi Mungu Haamini! Haamini! Haamini! Akaulizwa: Nani ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ni yule ambaye kwamba majirani zake hawasalimiki na shari zake].

Miongoni mwa sura za kuwaudhi majirani ni kuwaudhi watoto wake, kuchezea milki yake kuinua sauti kama ya nyimbo na kumpangisha mtu asiyeridhika nae.

Na kuwaudhi majirani kama kuwafanyia khiyana, kuwachunguza, kufuatilia aibu yake, kuangalia maharimu zake, kupitia dirisha lake au kumtembelea mke wake. Imetolewa onyo kali kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) kwa mwenye kufuatilia aibu za jirani zake, Ibnu Masoud alimueleza Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akisema: Ni dhambi gani kubwa? Ni kumkirisha Mwenyezi Mungu, kisha akasema ni dhambi gani? Akasema Mtume: ni kumuua mtoto wako kwa kuchelea kutomlisha, kisha akasema dhambi gani? Akasema ni kuzini pamoja na jirani yako”. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Kuzini mtu na wanawake kumi ni bora kuliko kuzini na mwanamke wa jirani yake].

Mcheni Mwenyezi Mungu, Enyi wenye kukhini jirani zenu ima kwa kuwapigia simu au kwa njia ya ujumbe au kwa njia ya kuangaliana. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

يقول الله سبحانه وتعالى) : وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُبِينًا ) [الأحزاب: 58]

{{Na wale wanaowaudhi wanaume Waislamu na wanawake Waislamu pasipo wao kufanya kosa lolote, bila shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi zilizo dhahiri}}.

Khutba ya pili

Enyi waja wa Mwenyezi Mungu kuwaudhi majirani kuna namna nyingi kama zifuatazo; kutumia milki ya jirani mwenzake kwa kumuudhi mfano wake kuegemea matagaa ya mti wake kwa jirani mwenzake, kufanya kiwanda ambacho kinatoa moshi au sauti au upepo ambapo kinaudhi majirani wenzake yapaswa kuzuiwa mfano wa madhara haya.

Tahadhari na Mambo ya Futayo:-

Kuwakodisha majirani wasio swali wala wasio muogopa Mwenyezi Mungu

Kukodi duka au sehemu ya kuuza vitu vya haramu kama kaseti za nyimbo na nyenginezo

Kumzuia jirani kutoshughulika kwa milki ya jirani mwenzake kama kuweka mbao katika ukuta wa jirani mwenzake.

Kuwakataza jirani wenzake kunufaika kwa mambo ya shirika ya watu wote mfano wake kuteka maji katika kisima au mto. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): Watu ni washirika kwa mambo matatu:-

Maji

Moto

Nyasi

Kuweka udhia katika njia.

Mcheni Mwenyezi Mungu na mbadilishane manufaa kati yenu na jirani zenu. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى): وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَى وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ( [المائدة: 2] {{Na saidianeni katika wema na twaa, wala msiaidiane katika dhambi na uadui}}

Mfano Mwema wa Waja Wema Waliopita na Jirani Zao

Tarekhe ya kiislamu imejaa mifano iliyokuwa ya juu kwa namna ya kuamiliana kati ya majirani. Imamu Dhahabi ametaja katika kitabu chake kwamba jirani wa Abi Hamza na huyu ni Walid Ibnu Kassim Bin Walid Hamdani ameulizwa Ahmad Ibni Hanbal akasema ni mwaminifu, na akaulizwa Abi Yaala akasema ni mtu bora na yeye ni jirani yetu tangu miaka hamsini iliopita na hatukumuona isipokuwa na kheri.

Ndugu katika imani, huo ni mifano ya watu wema waliopita namna walivyo ishi na majirani kwa wema na kusaidiana. Ni jukumu letu kuwaigiza watu wema na kufuata vitendo vyao, kwani huko ndiko kufaulu. Amesema Mshairi: Jifananisheni na watu wema hata kama hamtafanana nao, lakini kule kujifananisha nao ni kufaulu. Enyi Waumini fanyeni bidii kutekeleza haki za jirani kama alivyo tufundisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Mwisho

Ndugu Waislamu, tumeona wazi namna ya sheria ya Kiislamu ilivyo himiza juu ya haki za jirani. Na adhabu kali kwa wale watakao kiuka haki hizo. Kwasababu, mwanadamu ni lazima atekeleze haki mbili; haki ya kwanza ni ya Allah, na haki ya pili ni ya viumbe wenzake. Haki ya Allah anaweza mwanadamu kupata msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Yeye ni mwingi wa kusamehe. Lakini haki za mwanadamu ni lazima kutekeleza hapa duniani na ukishindwa, utadaiwa siku ya kiama. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Atuwezeshe kutekeleza haki zote zake na za viumbe vyake.

 





Vitambulisho: